Chelsea imekubali kumuuza Andre Schurrle ili kutunisha mfuko wa kumsainisha mshambuliaji Juan Cuadrado (pichani juu kushoto) kutoka Fiorentina.
Hatua ya Chelsea kumsajili Cuadrado, 26, nyota wa Colombia inaweza kukamilika muda mfupi ujao na kuwahi mechi ya kufa na kupona dhidi ya Manchester City wikiendi hii.
Chelsea inataka pauni milioni 30 kwa Schurrle, 24, na Wolfsburg ya Ujerumani inaongoza mbio za kumrejesha nyumbani mshambuliaji huyo, Borussia Dortmund nayo pia inamtaka.
Jose Mourinho si mshambiki wa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani, lakini anajua thamani yake sokoni. Mshindi huyo wa Kombe la Dunia anataka kurejea nyumbani.
Chelsea haina haraka ya kumuuza Schurrle (pichani chini) lakini imekuwa ikitamfuta mbadala wake ambapo Cuadrado na Douglas Costa ndio walengwa wakuu.
Kama dili la Schurrle litakamilika basi Chelsea itazitumia pesa hizo kumsajili Cuadrado ambaye ana kipengele cha pauni milioni 26.8 kwa klabu inayotaka kuvunja mkataba wake.
Comments
Post a Comment