Jose              Mourinho na  Diego Costa wakizungumza wakati wa mechi dhidi              ya Liverpool
          Jose              Mourinho amenuna baada ya chama cha soka England, FA kusema              kinamtoza faini Diego Costa kwa kuonesha mchezo usiokuwa wa              kiungwana.
          Mourinho              ameichukia FA na anaamini mfungaji wake anayeongoza              kufumania nyavu ametolewa kama mbuzi wa kafara kufuatia              kumchezea vibaya beki wa Liverpool, Emre Can.
          Kocha              huyo wa Chelsea ambaye amewahi kutozwa faini na FA alitakiwa              kuwa na mkutano na waandishi wa habari kesho ijumaa kuelekea              mechi ngumu dhidi ya Manchester City jumamosi, lakini              ameufuta.
        Diego Costa alionekana              kumkanyaga mguu wa kulia  Emre Can kwenye mechi ya nusu              fainali ya Capital One dhidi ya  Liverpool
        Costa              anaweza kufungiwa mechi tatu baada ya kutozwa faini na FA              kutokana na kitendo hicho alichomfanyia Can.
          Klabu              ya Chelsea imefuta ratiba ya mkutano na waandishi wa habari              na hatawathubutu hata kumtuma kocha msaidizi, Steve Holland              kuzungumza na vyombo vya habari.
          Imethibitishwa              kuwa kikao cha nidhamu cha FA kitakachokaa kesho              kitamuadhibu Costa.
          Licha              ya Costa kukataa kosa lake, mshambuliaji huyo wa Chelsea              anatarajia kufungiwa mechi tatu kuanzia ya jumamosi dhidi ya              Man City.
        
Comments
Post a Comment