JERMAIN DEFOE AREJEA BARCLAYS PREMIER LEAGUE … Sunderland yamtia mkononi


JERMAIN DEFOE AREJEA BARCLAYS PREMIER LEAGUE … Sunderland yamtia mkononi

Jermain Defoe is closing in on a return to English              football with a move to Sunderland

Jermain Defoe yuko mbioni kurejea Barclays Premier League baada ya kukubali kujiunga na Sunderland.

Kama ilivyofichuliwa na Sportsmail Jumatatu, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32, anajiandaa kuhitimisha miezi yake 11 aliyoitumika Toronto FC katika ligi kuu ya Marekani (Major League Soccer) na sasa anatua katika kikosi cha Gus Poyet.

Sunderland iko mbele kwa pointi moja mbele ya timu zilizoko kwenye janga la kushuka daraja baada ya kumudu kupachika magoli 18 tu msimu huu.

Defoe ametupia wavuni mabao 11 katika mechi 16 alizocheza MLS na sasa amedhamiria kurudi nyumbani.

Hull City nao walikuwa kwenye mbio za kunasa saini ya mshambuliji huyo wa zamani wa Tottenham, lakini Sunderland wanaonekana ndiyo washindi.



Comments