Mwimbaji na mtunzi tegemeo wa Mashujaa Band, Edward Antony maarufu kama Jado FFU au Chocolate ya warembo, anashuka na nyimbo mpya kali kama zawadi ya mwaka mpya kwa mashabiki wa bendi yao.
Akiongea na Saluti5 Jado ambaye pia ni mahiri katika kukung'uta gitaa la bass, amesema nyimbo hizo ni miongoni mwa nyimbo mpya sita za Mashujaa ambazo zinafanyiwa mazoezi makali.
Jado ametaja ngoma hizo kuwa ni "Bongo Michongo" na "Zengwe la Jirani".
Comments
Post a Comment