HATIMAYE TAMASHA LA MUZIKI WA DANSI LA CDS LAFIKIA MAHALA PAKE …Malaika, FM, Msondo, Mapacha kuwasha moto Jumapili hii



HATIMAYE TAMASHA LA MUZIKI WA DANSI LA CDS LAFIKIA MAHALA PAKE …Malaika, FM, Msondo, Mapacha kuwasha moto Jumapili hii

CDS YAANDAA TAMASHA KUBWA LA MUZIKI WA DANSI JANUARI                25 …bendi nne jukwaa moja, taarab nayo imo

Lile tamasha kubwa la muziki wa dansi linaloandaliwa na kampuni bingwa ya kusafirisha vifurushi, City Delivery Service (CDS), sasa liko usoni ambapo Jumapili hii Januari 25 moto wa burudani utawaka jijini Dar es Salaam.

Tamasha hilo litakalofanyika kwenye viwanja vya TCC Chang'ombe, litashuhudia bendi nne kali zikisimama jukwaa moja na kuonyeshana ufundi, lakini kama vile hiyo haitoshi, kutakuwa pia na burudani ya muziki wa taarab.

Mratibu wa tamasha hilo, Khamis Dacota, ameiambia Saluti5 kuwa bendi zitakazotumbuiza ni FM Academia, Malaika Band, Mapacha Watatu na Msondo Ngoma Music Band.

Kwa upande wa taarab, Dacota amelitaja kundi jipya la Ogopa Kopa Classic Band chini ya Malkia Khadija Kopa, kuwa ndilo litakalosababisha buradani ya mambo ya kimwambao.

 "CDS inatimiza miaka 10 tangu kuzaliwa kwake, na hivyo kampuni hiyo chini ya mkurugenzi wake Masoud Wannani (pichani juu), imeamua kufanya sherehe kubwa itakayoandamana na tamasha hilo la muziki wa dansi pamoja na mambo mengine kem kem," alisema Khamis Dacota.



Comments