HATIMAYE ABDUMALICK AREJESHWA KAZINI, APANDA JUKWAA LA MASHAUZI CLASSIC MANGO GARDEN


HATIMAYE ABDUMALICK AREJESHWA KAZINI, APANDA JUKWAA LA MASHAUZI CLASSIC MANGO GARDEN
HATIMAYE ABDUMALICK AREJESHWA KAZINI, APANDA JUKWAA LA            MASHAUZI CLASSIC MANGO GARDEN

Hatimaye mwimbaji wa kiume wa Mashauzi Classic Modern Taarab, Abdulmalick Shaaban "Rais wa Walemavu" ambaye alisimamishwa kazi amerejeshwa mzigoni na jana alipanda jukwaani Mango Garden kama anavyoonekana pichani juu.

Abdumalick alijiondoa Mashauzi Classic mwezi Disemba mwaka jana baada ya kukerwa na adhabu ya kusimamishwa kazi kwa muda usiojulikana.

Kisa cha kusimamishwa kazi ni kuondoka kwake na kwenda kufanya onyesho mkoani bila ruhusa na huku bendi yake nayo ikiwa na ratiba ya maonyesho.

Mwimbaji huyo kupitia mitandao ya kijamii akatangaza kuacha kazi, lakini wiki hii akaomba msamaha ili arejeshwe kazini.

Jana mwimbaji huyo alikuwepo Mango Garden ambapo alipanda jukwaani na kuimba wimbo wake "Sitosahu Yaliyonikuta"

Baadae Abdumalick aliiambia Saluti5 kuwa kwa wale wote wanaomkejeli kwa kuomba kwake msamaha, angependa wafahamu kuwa ajuaye maumivu ya jeraha ni mwenye jeraha mwenyewe.

Meneja wa Mashauzi Classic, Sumaraga, aliithibitishia Saluti5 kuwa Abdumalick amesamehewa na amerejeshwa rasmi kazini.



Comments