Mmoja wa waimbaji bora wa kiume katika miondoko ya taarab, Hashim Said "Mzee wa Majanga" kutoka Mashauzi Classic, yuko mbioni kukamilisha wimbo wake mpya utakaojulikana kama "Tuacheni Tulale"
Wimbo huu ni utunzi wake mwenyewe Hashim Said, songi la mahaba lenye mashairi matamu huku likikolezwa na sebene za hatari.
Huu unakuwa ni wimbo wa tatu kwa Hashim Said ndani ya Mashauzi Classic, lakini ndio utunzi wake wa kwanza katika kundi hilo.
Nyimbo zake mbili za awali ni "Niacheni Nimpende" na "Mimi ni Mwanaume" ambazo zote zimefanya vizuri sokoni.
Hashim Said ameimbia Saluti5 kuwa wimbo huo ni zawadi nzuri kwa mashabiki wa taarab, itakayowakumbusha kuwa yeye pia ni mtunzi mahiri.
Comments
Post a Comment