Aliyekuwa Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa, Godfrey Lebejo Ngereza amethibitishwa kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza hilo kuanzia tarehe 16 January 2015. Uthibitisho huo umefanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kupitia kifungu namba 5 (1) cha Sheria namba 23 ya mwaka 1984 iliyolianzisha Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)
Ngereza ameanza rasmi kazi hiyo tarehe 23 January 2015, baada ya kukaimu nafasi hiyo kuanzia mwaka 2013
Godfrey Mngereza ana shahada ya uzamili (MA) katika masuala ya Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na aliwahi kuwa Mwalimu wa Chuo Kikuu hicho katika Idara ya Sanaa na Sanaa za Maonesho (FPA) hadi mwaka 2008 alipoajiriwa rasmi na BASATA.
Comments
Post a Comment