- Get link
- X
- Other Apps
MICHUANO                ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2015 imeanza kutimua vumbi                nchini Guinea ya Ikweta kwa mechi mbili za kundi A kupigwa                siku ya ufunguzi.
          Mechi                ya kwanza iliyoanza majira ya saa 1:00 usiku jana, wenyeji                Guinea ya Ikweta walilazimisha sare ya kufungana bao 1-1                na Congo Brazaville.
          Guinea                ndio walikuwa wa kwanza kuandika bao katika dakika ya 17                kupitia kwa Emilio Nsue, lakini Congo walisawazisha dakika                ya 87' kupitia Thievy Bifouma.
          Mechi                ya pili iliyomalizika iliyoanza saa 4:00 usiku, Gabon                walipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Burkina Faso.
          Mabao                ya Gabon yalifungwa na Pierre-Emerick Aubameyang katika                dakika ya 19 na Malick Evouna katika dakika ya 72.
          Kwa                matokeo hayo, Gabon wanaongoza kundi A wakiwa na pointi 3                ambapo wamecheza mechi moja, wameshinda moja na                hawajafungwa.
          Nafasi                ya pili inashikwa na Gabon wanaofanana kwa kila kitu na                Congo Brazaville katika nafasi ya tatu.
          Wote                wamecheza mechi moja, wametoa sare moja, wamefungana goli                moja moja.
          Burkina                Faso wanaburuza mkia katika kundi A baada ya kufungwa                mechi yao ya kwanza usiku huu.
        - Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment