FM ACADEMIA KUVAMIA NGOME YA MALAIKA BAND MANGO GARDEN IJUMAA HII …CD za Chuki ya Nini kutolewa bure
Wazee wa Ngwasuma FM Academia, Ijumaa hii watakuwa Mango Garden Kinondoni kwenye ngome ya Malaika Band ambapo kutakuwa na 'sapraiz' kibao.
Malaika ambao hutumbuiza kila Ijumaa Mango Garden, watakuwa maeneo ya Chanika kwenye ukumbi wa Check Point – Pugu Kajiungeni.
Msemaji wa FM Academia Kelvin Mkinga, ameiambia Saluti5 kuwa bendi yake itakuwa na 'sapraiz' kibao ikiwemo utambulisho wa nyimbo mpya kabisa za albam yao ijayo.
Kama vile hiyo haitoshi, Kelvin amesema CD za albam ya Chuki ya Nini zitatolewa kama zawadi kwa kila mtu atakayekata tiketi.
Comments
Post a Comment