Haya ni mambo ya kawaida kwa wasanii kusalimiana kisanii. Usiku wa kuamkia leo rapa wa Mashujaa Band, Ferguson alipanda jukwaa la Extra Bongo na kufanya makamuzi makubwa
Ilikuwa majira ya saa 7.30 za usiku katika ukumbi wa Flamingo Magomeni ambapo Ferguson alipanda jukwaani na kushiriki kutumbuiza kwenye wimbo "Mtenda Akitendewa".
Kama inavyokumbukwa, Ferguson alishiriki kurekodi wimbo huo enzi hizo akiwa na Extra Bongo na hivyo kupanda kwake jukwaani kulisaidia kurejesha uhalisia wa wimbo huo hasa katika eneo la rap, eneo ambalo Ferguson alilitendea haki sana.
Comments
Post a Comment