FALCAO HATAFULIA HATA KAMA MANCHSTER UNITED WATAMTEMA, ASEMA WAKALA WA MSHAMBULIA HUYO



FALCAO HATAFULIA HATA KAMA MANCHSTER UNITED WATAMTEMA, ASEMA WAKALA WA MSHAMBULIA HUYO

Radamel Falcao has struggled at Man United and there              are doubts the striker will remain at Old Trafford

Radamel Falcao atakuwa kwenye "moja ya timu kubwa duniani" msimu ujao hata kama Manchester United haitamsajili mshambuliaji huyo wa Colombia.

Kiwango cha mkali huyo mwenye umri wa miaka 28 bado hakijakaa sawa tangu ajiunge na kikosi cha Louis van Gaal kwa mkopo kutoka Monaco ya Ufaransa.

Ameanza mechi nane na kufunga mabao matatu na sasa kumekuwa na mashaka kama kweli Manchester United itaamua kumchukua jumla Falcao.

Lakini wakala wa Falcao, Jorge Mendes amesema mchezaji wake ataondoka Monaco majira ya kiangazi na kujiunga na timu kubwa.

"Ni mchezaji mzuri sana, mashabiki wa Manchester United wamepata mchezaji wa hali ya juu," alisema Mendes katika mazungumzo yake na Sky Sports Italia.

"Anaweza kucheza timu yoyote, chochote kinaweza kutokea. Kwa asilimia mia moja, atakuwa katika moja ya timu bora duniani, hata kama haitakuwa Manchester United. Ni suala la kuvuta subira, tutaona nini kitatokea



Comments