FABREGAS AWEKA REKODI MPYA YA UPISHI WA MAGOLI BARCLAYS PREMIER LEAGUE …asogelea pia rekodi ya Thierry Henry


FABREGAS AWEKA REKODI MPYA YA UPISHI WA MAGOLI BARCLAYS PREMIER LEAGUE …asogelea pia rekodi ya Thierry Henry

Cesc Fabregas has become the first player in Premier                League history to get 15 assists in two seasons

Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas amekuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Barclays Premier League kusaidia kupika magoli 15 (kutoka pasi zilizozaa goli) katika misimu miwili tofauti.

Nyota huyo wa zamani wa Arsenal amepika bao lake la 15 tangu ajiunge na Chelsea akitokea Barcelona majira ya kiangazi wakati timu yake ikiifunga Swansea 5-0 katika dimba la Liberty Stadium siku ya Jumamosi.

Fabregas alianza kuweka rekodi msimu wa 2007-08 akiwa na Arsenal ambapo alichangia magoli 17 wakati vijana wa Arsene Wenger wakimaliza katika nafasi ya tatu nyuma ya Chelsea na mabingwa Manchester United.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania sasa anavizia rekodi ya Thierry Henry aliyoweka miaka 12 iliyopita ya kutoa pasi zilizozaa magoli mara 20 kwa Arsenal.



Comments