Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Wapinzani wa Azam FC katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika mwaka huu, E-Merrikh wametuma salamu Chamazi baada ya kuwafumua mabingwa wa Uganda KCC FC mabao 2-1 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki mjinI Khartoum, Sudan jana.
Wenyeji walipumzika wakiwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Bakri Almadina na Mkenya Allan Wanga lakini walifungwa bao moja kipindi cha pili na mtokeabenchi Michael Birungi.
Mechi hiyo ilikuwa maalum kuzipasha misuli kabla ya kuanza kwa hatua ya awali ya Klabu Bingwa Afrika katikati ya mwezi ujao, mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu ya Sudan El-Merikh wakiivaa Azam FC jijini Dar es Salaam wakati KCC FC ikivaana na Cosmos De Bafia ya Cameroon.
Azam FC baada ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Simba mwishoni mwa wiki, watakwea pipa kwenda DRC kushiriki michuano maalum ya kimataifa ikiwa ni sehemu ya mikakati yao ya kuipashia misuli El-Merrikh ambayo imetoka kambini Qatar ikijipima na timu ngumu ya Schalke 04 ya Ujerumani.
Wiki mbili zilizopita, El-Merrikh ilituma shushushu Zanzibar kuisoma Azam FC wakati wa michuano ya Kombe la Mapinduzi mwaka huu.
Comments
Post a Comment