DRC, TUNISIA ZATINGA ROBO FAINALI AFCON 2015




DRC, TUNISIA ZATINGA ROBO FAINALI AFCON 2015
Zambia wakikwaana na Cape Verde leo.
TIMU za Tunisia na DR Congo zimefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali Afcon 2015 kutoka Kundi B huku Cape Verde na Zambia zikiaga mashindano hayo yanayoendelea huko Equitorial Guinea.
DRC wakimenyana na Tunisia.
Timu hizo zimetinga hatua hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wao wa mwisho uliopigwa leo huku Zambia na Cape Verde wakitoka suluhu na kuondolewa.
Zambia na Tunisia wameungana na Congo pamoja na Equitorial Guinea waliokata tiketi zao za robo fainali jana kutoka Kundi A.
Tunisia wamemaliza wakiwa vinara wa Kundi B kwa kuwa na pointi 5 huku DR Congo wakiwa nafasi ya pili na pointi zao 3.
Kesho Senegar watamenyana na Algeria huku Ghana wakikwaana na Afrika Kusini katika kusaka tiketi ya kutinga robo fainali kutoka Kundi C.


Comments