DISCO JIPYA KUFUNGULIWA LEO MACHINGA COMPLEX …kuandamana na party ya mwaka mpya ya Twanga Pepeta



DISCO JIPYA KUFUNGULIWA LEO MACHINGA COMPLEX …kuandamana na party ya mwaka mpya ya Twanga Pepeta
DISCO JIPYA KUFUNGULIWA LEO MACHINGA COMPLEX …kuandamana            na party ya mwaka mpya ya Twanga Pepeta

Kuna kitu kipya kinaanzishwa leo jijini Dar es Salaam ndani ya ukumbi wa Business Lounge pale Machinga Complex Ilala nyuma ya Uwanja wa Karume.

Ni disco jipya kabisa litakalojulikana kama Muziki Bambataa, ngoma za kiafrika zikitarajiwa kuchukua nafasi zaidi.

Unamkumbuka Prince Baina Kamukulu aliyetamba na kipindi cha Afrika Bambataa cha Clouds FM? Basi huyo atakuwa ni mmoja wa wasasabibishaji wa disco hilo litakalokuwa linarindima hapo Business Lounge kuanzia Ijumaa hii na kila Ijumaa.

Saluti5 imefahamishwa kuwa kwa leo disco hilo ni bure kabisa ikiwa ni maalum kwa wadau wa muziki wa disco na pamoja na wale muziki wa dansi.

Lakini mbali na disco hilo, ndani yake kutakuwa pia na party ya kukaribisha mwaka mpya kwa Twanga Pepeta.

Wasanii wote wa Twanga Pepeta watakuwepo hapo kulicheza disco hilo na kufurahia kuanza kwa mwaka mpya.

Siku zote umekuwa ukiwaona Twanga Pepeta jukwaani, lakini leo utajumuika nao kama wananchi wa kawaida, hawatatoa burudani yoyote zaidi ya kusakata disco na kupata nasaha kidogo kutoka kwa baadhi ya wanamuziki hao.



Comments