Ukiskia mtu kapigwa mkono mzima maanake kachukua 5-0, Chelsea inachanua kileleni kwa kuitandika Swansea bao tano bila majibu katika mechi ya upande mmoja ya Ligi Kuu ya England.
Hadi mapumziko Chelsea ilikuwa inaongoza 4-0 kwa mabao ya Diego Costa na Oscar ambao kila mmoja alitupia wavuni magoli mawili.
Andre Schurrle akafunga bao la tano dakika 79 kiasi cha dakika tatu tu tangu aingie uwanjani kuchukua nafasi ya Willian.
Swansea City (4-4-2):Fabianski 5; Tiendalli 4, Fernandez 4, Williams 4.5,Taylor 4.5; Dyer 4 (Barrow 74), Carroll 4, Sigurdsson 5, Routledge 5.5 (Emnes 32, 5.5), Oliveira 4.5 (Fulton 66, 5); Gomis 5.
Chelsea (4-2-3-1): Cech 6; Ivanovic 6.5, Cahill 6, Terry 6, Luis 6, Matic 7, Fabregas 7.5 (Ramires 74, 6), Willian 7.5 (Schurrle 76), Oscar 8.5, Hazard 7; Costa 8 (Remy 74, 6).
Comments
Post a Comment