Cristiano Ronaldo amekula kadi nyekundu baada ya kumpiga ngumi ya uso beki wa Cordoba, Jose Angel Crespo lakini bado Real Madrid ikafanikiwa kutwaa pointi tatu muhimu.
Real Madrid ikaendelea kung'ang'ania kileleni mwa La Liga baada ya kuibanjua Cordoba 2-1 kwa magoli ya Benzema na Gareth Bale.
Cordoba walikuwa wa kwanza kupata goli mfungaji akiwa Ghilas kwa njia ya penalti kunako dakika ya tatu, Benzima akachomoa dakika ya 27.
Ronaldo alilambwa kadi hiyo dakika ya 82 na hivyo kumwachia Gareth Bale majukumu yote ya kupiga mipira ya adhabu ikiwemo penalti ya dakika ya 89 iliyozaa bao la ushindi.
Cordoba: Martin Corral, Gunino, Pantic, Crespo, Fraga, RodrÃguez Barrera, Rossi, Bebe, Nicolas Cartabia, Ghilas, Andone (Vico Villegas 80)
Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Ramos, Marcelo (Fabio Coentrao 72), Khedira (Illarramendi 64), Kroos, RodrÃguez (Jese 80), Bale, Benzema, Ronaldo.
Comments
Post a Comment