CHELSEA YAIBANJUA LIVERPOOL 1-0 'EXTRA TIME' NA KUTINGA FAINALI YA CAPITAL ONE CUP …Diego Costa vurugu tupu
Chelsea imeifunga Liverpool 1-0 na kutinga fainali ya Capital One Cup kwa jumla ya bao 2-1 kufuatia sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita.
Dakika ya 4 ya muda wa lala salala (90+4) beki Branislav Ivanovic akaifungia Chelsea bao pekee baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya mpira wa adhabu uliopigwa na Willian.
Wakati Chelsea iliyokuwa nyumbani, ikimiliki zaidi mpira kipindi cha kwanza, ni Liverpool ndiyo iliyopoteza nafasi nyingi za wazi katika kipindi hicho.
Mshambuliaji tegemeo wa Chelsea Diego Costa licha ya kung'ara lakini alionyesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu.
Costa alicheza mpira wa kibabe na mara nyingi alihusika katika kila 'vurugu' iliyotokea dimbani.
Mshambuliaji huyo alikuwa na bahati kutolimwa kadi nyekundu kwa kumsigina kwenye 'enka' beki Emre Can jirani kabisa na benchi la waamuzi wa akiba mwanzo tu mwa kipindi cha kwanza.
Lakini Costa huyu huyo akamsigina tena beki mwingine wa Liverpool, Martin Skrtel kwa staili ile ile lakini safari hii ikiwa ni kipindi cha pili na bado akaendelea kunusurika na kadi nyekundu.
CHELSEA: Courtois 7.5, Ivanovic 6.5, Zouma 6, Terry 6.5, Luis 6 (Azpilicueta 78), Fabregas 6 (Ramires 50), Matic 6, Willian 7 (Drogba 119), Oscar 6.5, Hazard 8, Costa 7.5.
LIVERPOOL: Mignolet 7.5, Can 6, Skrtel 7, Sakho 6.5 (Johnson 57), Markovic 6 (Balotelli 70), Henderson 7, Lucas 7.5, Moreno 7 (Lambert 105), Coutinho 8, Gerrard 6, Sterling 7.5.
Comments
Post a Comment