HABARI zilizotufikia mchana huu ni kuwa mwanamuziki Peter Kanuti amefariki kwa ajali ya gari huko Zanzibar, ambapo tairi la gari limemeponda kichwa. Peter ni kutoka katika familia iliyo na wanamuziki wengi. Ukianzia na kaka yao marehemu Gaspar Kanuti aliyekuwa mpiga gitaa mahiri nchini, kuna wapiga magitaa wengine kama Fred na Joseph Kanuti. Kwa vile katika siku za mwisho alikuwa katika Taarab ya jeshi la Magereza Zanzibar, wao ndio wanawasiliana na ndugu kujua mipango ya mazishi
MUNGU AMLAZE PEMA PEPONI
Comments
Post a Comment