Daley              Blind aliifungia goli timu yake  dhidi ya West Bromwich              Albion  
          VIDEO              za Daley Blind zimewekwa You Tube zikionesha magoli ya ajabu              aliyofunga, ujuzi, pasi na 'Tackles' anazopiga.
          Ukweli              ni kwamba video hizo zimejumuisha na goli moja aliloifungia              Manchester United United dhidi ya West Brom mwezi Oktoba              mwaka jana.
        Blind              akipozi katika picha na jezi yake baada ya kujiunga na              Manchester United, akiungana na  Louis van Gaal na Radamel              Falcao.
          Blind              jana amekutana na waandishi wa Uingereza na aliulizwa kuhusu              maoni ya Gary Neville ambaye alisema hachezi vizuri,              anacheza sana pasi mraba ambazo hazina madhara kwa              wapinzani.
           Akizungumzia              maneno hayo ya nahodha huyo wa zamani wa Manchester United,              Blind amekiri kuyasikia vizuri.
          "Kiukweli,              nilimsikiliza lakini najaribu kucheza mchezo wangu na vile              anavyotaka mwalimu ambapo anataka kumiliki mpira".
          "Siku              zote kuna wanaotaka kuwazungumzia walimu au timu, vinginevyo              TV zao hazitakuwa na mvuto".
          "Naweza              kuchukua kidogo ukosoaji. Watu wa TV wanasema wanachotaka.              Unasikiliza, lakini nadhani nimecheza vizuri kwenye baadhi              ya mechi"
        
Comments
Post a Comment