Gerard Pique amesherehekea vizuri mechi yake ya 200 kwa Barcelona baada ya kuifungia bao moja katika ushindi mnono wa bao 6-0 dhidi ya Elchie.
Katika mchezo huo wa upande mmoja wa La Liga, Pique alifungua kitabu cha magoli kwa bao la dakika ya 36.
Magoli mengine ya Barcelona yalifungwa na Messi dakika ya 54 (kwa penalti) na 88, Neymar 69, 71, Pedro 90+2.
Mshambuliaji Luis Suarez ambaye amekuwa na ukame wa magoli tangu ajiunge na Barcelona kutokea Liverpool, hakupata bahati kucheza katika mechi hii ambayo pengine ingemsaidia kuongeza akaunti yake ya magoli.
ELCHE (4-4-2): Tyton; Suarez, Roco, Pelegrin, Cisma (Albacar Gallego, 61); Gonzalez Morales (Rodríguez Lomban, 70), Pasalic, Rodríguez Romero, Fajr; Niguez Esclapez, Jonathas de Jesus
BARCELONA (4-3-3): Bravo; Montoya, Pique, Bartra, Alba (Busquets, 70); Xavi (Sergi, 72), Mascherano (Adriano, 70), Rafinha; Pedro, Messi, Neymar
Comments
Post a Comment