Lionel Messi ameipatia Barcelona ushindi mwembamba katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Copa del Rey Jumatano usiku dhidi Atletico Madrid.
Barcelona walizawadiwa penalti zikiwa zimesalia dakika nne kabla ya mpira kumalizika na ingawa Messi alishuhudia penalti yake ikiokolewa na kipa Jan Oblak, lakini bado aliwahi kwenda kuusukumiza wavuni mpira huo uliookoiewa na kuipatia Barcelona bao pekee.
Atletico Madrid waliokuwa ugenini, walifanikiwa kuwabana Barcelona kwa sehemu kubwa ya mchezo na kuwafanya washindwe kabisa kupanga mashambulizi, lakini hata hivyo bahati haikuwa upande wao.
BARCELONA (4-3-3): Ter Stegen; Alba, Alves, Piqué, Mascherano; Rakitic (Xavi 77), Busquets, Iniesta (Bartra 87); Suárez, Messi, Neymar
ATLETICO MADRID (4-4-2): Oblak; Juanfran, Miranda, Godin, Siqueira; Mario Suarez, Gabi (Jimenez 88), Koke, Arda; Griezmann (Garcia 66), Torres (Mandzukic 46).
Comments
Post a Comment