Kwa mara ya pili mfululizo, kuumwa kumemfanya Mario Balotelli ashindwe kwenda uwanjani kuichezea Liverpool na kujikuta akiutazamia nyumbani mchezo wa FA kati ya timu yake dhidi ya Chelsea.
Mchezaji huyo mtukutu akatupia picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ikimuonyesha akiwa sebuleni kwake akitazama mchezo huo ulioishia kwa sare ya 1-1.
Balottelli akaandika: "Kuumwa kunaweza kunifanya nishindwe kuisaidia timu yangu uwanjani lakini hakutanizuia kuisapoti timu yangu nje ya uwanja."
Comments
Post a Comment