BAADA YA KUUGUA KWA MIEZI MIWILI HATIMAYE SHAABAN DEDE AREJEA JUKWAANI ...pata picha zake pamoja na wadau
Hizi ni habari njema kwa mashabiki wa Msondo Ngoma Music Band, mwimbaji na mtunzi tegemeo wa bendi hiyo Shaaban Dede amerejea jukwaani baada ya kukosekana kwa muda mrefu.
Dede yuko jukwaa la Msondo usiku huu ndani ya Leaders Club ikiwa ni onyesho lake la kwanza tangu ugonjwa wa sukari umlaze kitandani kwa miezi miwili.
Mwimbaji huyo mwenye sauti tamu kupindukia alikuwa na hali tete na hakuweza kuhudhuria kazini hata mara moja katika kipindi chote hicho cha miezi miwili.
Mashabiki wa Msondo waliofika Leaders walishangilia kumuona Dede akiwajibika jukwaani kwa ubora ule ule huku afya yake ikonekana iko swafi kabisa.
Dede ameiambia Saluti5 kuwa hali yake ni nzuri na anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kurejea tena kazini.
Comments
Post a Comment