ARSENAL YAPEWA RUNGU …GABRIEL PAULISTA SASA RUKSA KUSALIWA EMIRATES, KIBALI CHEKE CHA KUFANYA KAZI ENGALAND SI TATIZO TENA
Arsenal imehakikishiwa kibali cha kufanya kazi kwa sentahafu wa Villareal, Gabriel Paulista na sasa wanaweza wakakamilisha usajili wake wa pauni milioni 11.2.
Gabriel Paulista mwenye umri wa miaka 24 hajawahi kuichezea timu ya taifa ya Brazil, jambo lililokuwa linafanya upatikanaji wa hati ya kufanyia kazi England uwe mgumu lakini sasa beki huyo ameambiwa kibali si tatizo tena kwake.
Kanuni zilikuwa zinasema kuwa ni wachezaji ambao wamecheza asilimia 75 ya mechi za kimataifa dhidi ya nchi zilizoko katika 70 bora ya viwango vya FIFA ndani ya miaka miwili ndiyo watakaofaulu kupata vibali vya kazi England.
Paulista anakamilisha vipimo vya afya kabla ya kutangazwa rasmi Emirates, dili lake linamfanya mshambuliaji chipukizi wa Arsenal Joel Campbell kwenda Villareal kwa mkopo kama sehemu ya makubaliano ya uhamisho wa beki huyo kisiki.
Joel Campbell ataitumikia Villareal hadi mwisho wa msimu huu.
Comments
Post a Comment