ARSENAL YAKARIBIA KUMSAJILI BEKI GABRIEL PAULISTA WA VILLAREAL …lakini ngoma ipo kwenye hati za kufanyia kazi England



ARSENAL YAKARIBIA KUMSAJILI BEKI GABRIEL PAULISTA WA VILLAREAL …lakini ngoma ipo kwenye hati za kufanyia kazi England

Defender Paulista is yet to make a senior appearance              for the Brazilian national side

Arsenal wako njiani kukamilisha usajili wa sentahafu wa Villareal, Gabriel Paulista lakini bado watakuwa na kibarua kigumu kuhakikisha wanapata hati za kufanyia kazi England kwa mchezaji huyo wa Kibrazil.

Hadi Jumatano washika bunduki hao walikuwa wamefikia pazuri katika harakati za kumnasa beki huyo ambaye kiwango chake cha kuuvunja mkataba wake Villareal ni pauni milioni 15.

Villarreal's Gabriel Paulista (right) could be heading              for Arsenal if they can secure a work permit

Lakini tatizo kubwa kwa Arsenal ni kupata kibali cha kufanyia kazi kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 24.

Gabriel Paulista hajawahi kuichezea timu ya taifa ya Brazil, jambo linalofanya upatikanaji wa hati ya kufanyia England kazi uwe mgumu.

Arsenal watalazimika kuthibitisha kuwa mchezaji huyo ana kipaji cha kipekee ili apate kibali huku akiwa hajawahi kuchezea timu ya taifa, moja ya sifa za lazima katika kupatiwa kibali England.

Kanuni zinasema wazi kuwa ni wachezaji ambao wamecheza asilimia 75 ya mechi za kimataifa dhidi ya nchi zilizoko katika 70 bora ya viwango vya FIFA ndani ya miaka miwili ndiyo watakaofaulu kupata vibali vya kazi England.



Comments