Arsenal imekamilisha usajili wa kiungo kinda Krystian Bielik kutoka klabu ya Legia Warsaw ya Poland kwa ada inayokisiwa kufikia pauni milioni 2.5
Kwa kupitia mtandao wao rasmi, Arsenal imethibitisha kumaliza dili la mchezaji huyo mwenye urefu wa futi sita na inaamini atakuwa hazina nzuri kwao.
Krystian Bielik mwenye umri wa miaka 17 anatua Arsenal baada ya kudumu kwa mwaka mmoja tu Legia iliyomsajili mwaka jana na kumpa mkataba wa hadi mwaka 2017.
Hapo kabla, Bielik alisema anakwena London kukamilisha ndoto yake. "Natumani nitakuwa mchezaji wa Arsenal hivi punde tu," alisema kinda huyo kupitia mtandano rasmi wa klabu ya Legia.
Bielik amecheza mechi sita katika kikosi cha kwanza cha Legia tangu alipojiunga nayo akitokea Lech Poznan – mechi tano za ligi na moja ya Europa League.
Kiungo huyo pia ni mmoja wa wachezaji tegemeo wa timu ya taifa ya Poland kwa vijana wa umri chini ya miaka 17.
Kiuchezaji, Bielik ni kiungo mkabali mwenye uwezo wa hali ya juu wa kucheza mipira ya vichwa. Inadaiwa kuwa anauwezo pia wa kucheza kama sentahafu.
Krystian Bielik anategemewa kutumika zaidi katika kikosi cha vijana wa Arsenal chini ya miaka 21 kabla ya kuingizwa jumla kwenye timu ya wakubwa.
Comments
Post a Comment