ALLY CHOCKY ASISIMUA MASHABIKI WA TWANGA PEPETA LEADERS CLUB …akamua nyimbo 4 kwenye jukwaa la Twanga

Wala hakuna aliyekumbuka kuwa wanayemuona jukwaani ni Ally Chocky aliyemtaka mmiliki wa Twanga Pepeta asihudhurie msiba wake pindi Mungu akimchukua, bali walimuona Ally Chocky waliyem-miss kwa miaka miaka mingi.

Hiyo ilikuwa ni Leaders Club Jumapili usiku wakati Ally Chocky alipopanda jukwaa la Twanga Pepeta na kusalimia kisanii kwa kuimba nyimbo nne …Mashabiki wa Twanga Pepeta wakapagawa.

Hii ni mara ya kwanza kwa Ally Chocky kupanda jukwaa la Twanga Pepeta tangu alipounda awamu ya pili ya Extra Bongo zaidi ya miaka mitano iliyopita.

Chocky akaimba nyimbo za "Mtaa wa Kwanza", "Password", "Furaha ya Harusi" na "Chuki Binafsi".

Nyimbo nyingine alidonyoa donyoa vipande muhimu, lakini ni "Password" ndio uliopigwa wimbo mzima na kuwafanya mashabiki wa Twanga wapate burudani iliyojaa kila aina ya hisia.

Comments