Mwimbaji wa kiume wa Mashauzi Classic Modern Taarab, Abdulmalick Shaaban ambaye alisimamishwa kazi lakini na yeye akatangaza kujiondoa kundini, amebadili mawazo na kuomba radhi uongozi wa kundi hilo. (Mwisho wa habari hii utamsikiliza alivyoongea).
Abdumalick alijiondoa Mashauzi Classic mwezi Disemba mwaka jana baada ya kukerwa na adhabu ya kusimamishwa kazi kwa muda usiojulikana.
Kisa cha kusimamishwa kazi ni kuondoka kwake na kwenda kufanya onyesho mkoani bila ruhusa na huku bendi yake nayo ikiwa na ratiba ya maonyesho.
Mwimbaji huyo kupitia mitandao ya kijamii akatangaza kuacha kazi.
Lakini msanii huyo ameiambia Saluti5 jana mchana kuwa ameomba radhi kwa uongozi na kwamba sasa anataka kurejea kazini.
Akiongeea katika ofisi za Saluti5, Abdulmalick akasema alishawishiwa vibaya na watu wasioitakia mema bendi.
"Nimeongea na meneja wa bendi Sumaraga na sasa nachosubiri ni jibu la kurejeshwa kazini, nimejifunza mengi katika muda wote huu niliokuwa nje ya kazi.
"Nimegundua kuna watu wako maalum kwaajili ya kuharibu maisha ya watu, wanakuongoza kwenye janga, ukishadumbikia huwaoni tena.
"Nina ahidi nitakuwa mtiifu kwa uongozi na kwa wasanii wenzangu, ," alisema Abdumalick ambaye hupenda kujiita Rais wa Walemavu.
Naye meneja wa Mashauzi, Sumaraga aliimbia Saluti5 kuwa ni kweli amepokea ombi la Abdulmalick na huenda muda si mrefu msanii huyo atarudishwa kundini.
"Haya ni maisha tu na wala hatupo kwaajili ya kukomoana, tunashughulikia suala lake katika mwelekeo mzuri," alisema Suma.
Hebu sasa msikilize hapo chini Abdulmalick alivyoongea na Saluti5.
Comments
Post a Comment