YANGA SC WASEMA WAMEPANIA KUSHINDA MECHI ZOTE TATU ZIJAZO DHIDI YA AZAM FC, MBEYA CITY NA COASTAL UNION
- Get link
- X
- Other Apps
Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Benchi jipya la ufundi la Yanga SC limepania kushinda mechi tatu mfululizo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) ili kujiweka pazuri katika msimamo wa ligi hiyo msimu huu, imefahamika.Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro, ameuambia mtandao huu jijini hapa leo kuwa lengo lao la kwanza baada ya kuingia madarakani rasmi wiki iliyopita ni kuhakikisha wanashinda mechi tatu zinazofuata dhidi ya Azam FC (Dar es Salaam Jumapili, Mbeya City FC (Mbeya Januari 3) na Coastal Union (Tanga) Januari 10).
"Benchi letu jipya la ufundi limeamua timu ikae kambini kwa kipindi chote cha mechi tatu zijazo. Tukishinda mechi zote hizo, tutakuwa tutakuwa katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi," amesema Muro, mwandishi bora wa habari nchini mwaka juzi.
Kikosi cha Yanga SC, mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, kwa sasa kiko chini ya Mdachi Hans van der Pluijm na msaidizi mzawa Boniface Wambura baada ya kufungashiwa virago kwa aliyekuwa kocha mkuu Mbrazil Marcio Maximo na msaidizi wake Leonardo Neiva wiki iliyopita baada ya kufungwa na Simba mabao 2-0 katika mechi ya 'ndondo ya 'Nani Mtani Jembe 2′.
Azam FC na Yanga SC zinakamata nafasi ya pili na ya tatu katika msimamo wa VPL zote zikiwa na pointi 13, mbili nyuma ya vinara Mtibwa Sugar FC lakini Azam inabebwa na mtiririko wa herufi katika nafasi ya pili baada ya kufanana kwa kila kitu na Yanga.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment