Na Bertha Lumala, Dar es Salaam
Mabingwa mara 24 wa Tanzania Bara, Yanga wataanza kwa kuwavaa SC Villa katika michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar mwakani.
Yanga SC ni miongoni mwa timu nne za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) zilizoalikwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kushiriki michuano hiyo mwakani.
Klabu nyingine za Bara zilizoalikwa ni Azam, Mtibwa Sugar na Simba zinazoungana na timu nyingine mbili kutoka Uganda SC Villa na mabingwa watetezi KCC FC, timu moja kutoka Kenya Ulinzi Stars na timu za Zanzibar KMKM, Shaba FC, Mtende Rangers, JKU FC, Police Zanzibar na Mafunzo.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amesema kikosi chao kitaivaa SC Villa iliyomkuza Emmanuel Okwi wa Simba SC katika mechi ya kwanza la kundi lao itakayochezwa Uwanja wa Amaan, Unguja Jumamosi.
Ratiba kamili ya michuano hiyo itatolewa rasmi kesho.
Comments
Post a Comment