YANGA BOTSWANA, AZAM YAPEWA EL-MARREIKH MICHUANO YA CAF


YANGA BOTSWANA, AZAM YAPEWA EL-MARREIKH MICHUANO YA CAF

Na Bertha Lumala, Dar es Salaam

MABINGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Azam FC wamepangwa kucheza dhidi ya El Marreikh ya Sudan katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika mwakani huku Yanga wakipewa timu ya BDF XI ya Botswana katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani mwakani.
Kwa mujibu wa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao ramsi wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo, droo ya michuano ya 19 ya Klabu Bingwa Afrika mwakani na michuano ya 12 ya Kombe la Shirikisho barani imechezeshwa kwenye makao makuu ya CAF jijini Cairo, Misri leo asubuhi, klabu 58 zikichuana katika Klabu Bingwa na 56 katika Kombe la Shirikisho.
gg
Michuano yote miwili ya bara itaanzia katika mechi ya awali zitakazochezwa kati ya Februari 13, 14 na 15 na kurudiana kati ya Februari 27, 28 na Machi Mosi mwakani.

Mechi za hatua ya kwana kuwania kuingia 16 bora (1/16 round) ziotachezwa kati ya Machi 13, 14 na 15 na kurudiana kati ya Aprili 03, 04 na 05 na hatua ya 8-bora kuamua nani anaingia hatua ya makundi zimepangwa kuchezwa kati Aprili 17, 18 na 19 kwa mechi za kwanza kurudiana kati ya Mei 01, 02 na 03.

Kwa michuano ya Kombe la Shirikisho, mechi za kwanza kusaka timu zitakazoingia hatua ya nane bora zitachezwa kati ya Mei 15, 16 na 17 na kurudiana kati ya Juni 05, 06 na 07.

Katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, mabingwa watetezi ES Setif hawajapangwa katika hatua ya awali pamoja na timu za Coton Sport, AC Leopards, Al Ahly, TP Mazembe na timu mbili za Tunisia, CSS na EST.

Timu ambazo hazijapangwa katika hatua ya awaliya mtoano katika michuano ya Kombe la Shirikisho, ni Asec Mimoas, Zamalek, Djoliba, na wanafainali wa Klabu Bingwa mwaka huu AS Vita, Orlando Pirates, Ahli Shendi na Club Africain ya Tunisia.

BDF XI kwa sasa iko nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu ya Botswana msimu huu ikiwa na pointi 28, tisa nyuma ya vinara Township Rollers. Timu zote 16 zinazoshiriki ligi hiyo zimecheza mechi 15.

Timu hiyo ya Jeshi la Ulinzi la Botswana (BDF) imetwaa taji la Ligi Kuu nchini humo mara saba 1981, 1988, 1989, 1991, 1997, 2002 na 2004 na imeshiriki mara sita michuano ya Klabu Bingwa Afrika huku ya juu zaidi waliyowahi kufika ni raundi ya kwanza 1982 na 1989, mara nyingine zote walitolewa hatua ya awali.



Comments