VAN GAAL ALIA NA RATIBA YA MECHI ZA CHRISTMAS NA MWAKA MPYA …asema mfumo huo unawachosha wachezaji na hauna tija
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal anaamini utamaduni wa soka la Uingereza kucheza mechi za papo kwa papo kati ya Christmas na mwaka mpya, unahatarisha ubora wa Barclays Premier League.
Kikosi cha Van Gaal kilionekana kuhitaji wazi mapumziko wakati kilipopambana na Tottenhm Jumapili, siku chache baada ya kuikabili Aston Villa.
Na sasa United inajiandaa kumenyana na Stoke City siku ya mwaka mpya kabla ya kujitosa tena uwanjani siku ya Jumapili kumenyana na Yeovil katika mchezo wa FA Cup.
Mdachi huyo amesema mchezaji hawezi kuimarika baada ya masaa 48 na kama vile hiyo haitoshi, akadai mfumo huo wa soka la Uingereza hauna tija.
Comments
Post a Comment