MSHAMBULIAJI Fernando Torres anatarajiwa kujiunga na klabu yake iliyomuibua kisoka, Atletico Madrid baada ya kufikia makubaliano
na AC Milan ambao watamchukua Alessio Cerci kutoka timu hiyo.
Milan imethibitisha katika Televisheni yake kwamba mazungumzo yamefanyika na makubaliano yamefikiwa, hivyo kinachosubiriwa
ni utekelezaji wake.
Torres yuko katika Mkataba wa mkopo wa miaka miwili kutoka Chelsea, lakini ameshindwa kuvutia Milan na Atletico wanashawishika kwamba El Nino anaweza kufufua makali yake
akirejea kucheza Hispania.
Waatauchukua wao Mkataba wa mkopo wa Chelsea na kumsaini
kwa miezi 18 Torres.
Africa Newss
Comments
Post a Comment