Tony Pulis amekataa nafasi ya kuwa kocha mpya wa Newcastle United, akihofia kuwa kikosi cha kwanza kitakuwa kikipangwa na kamati.
Kocha huyo wa zamani wa Stoke na Crystal Palace amewaambia washauri wake kuachana na mazungumzo na Newcastle baada ya kuingia hofu kuwa mmiliki mtata wa klabu hiyo, Mike Ashley na skauti mkuu wa kusaka wachezaji Graham Carr watakuwa wakiingilia upangaji wa timu.
Ashley na Carr walisimamia usajili wa wachezaji, hali ambayo Alan Pardew alikubaliana nayo. Lakini inaaminika ndiyo sababu iliyomfanya atimke na kujiunga na Crystal Palace.
Tony Pulis amekuwa hana kazi tangu alipoiacha Crystal Palace muda mfupi kabla Ligi Kuu haijaanza.
Comments
Post a Comment