SHIRIKISHO la soka Tanzania, TFF limelazimika kuahirisha mechi mbili kwa timu nne za ligi kuu Tanzania bara, Simba, Yanga, Azam fc na Mtibwa FC ili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi 2015 ambapo timu hizo zimealikwa kushiriki kuanzia januari mosi mpaka januari 13 mwakani.
Katika kikao cha jana baina ya TFF na klabu hizo, wawakilishi wa timu hizo kubwa nchini waligoma kucheza kombe la Mapinduzi huku wakiendelea na ligi kuu.
Awali TFF haikuhusisha kombe la Mapinduzi katika ratiba yake na ligi ilitakiwa kuendelea kama kawaida, lakini Serikali ya Zanzibar imetumia nguvu kuhakikisha timu za Bara zinashiriki.
Kwa maana hiyo, mechi baina ya Azam fc na Mtibwa Sugar fc iliyotakiwa kupigwa januari 3 haitakuwepo. Pia mechi ya Azam fc dhidi ya Kagera Sugar iliyotakiwa kuchezwa Januari 10 mwakani haitakuwepo.
Kwa upande wa Yanga, mechi yake ya januari 3 dhidi ya Mbeya City fc na januari 11 dhidi ya Coastal Union zimeahirishwa.
Mtibwa Sugar waliotakiwa kucheza januari tatu na Azam, halafu januari 11 na Tanzania Prisons, mechi zao zimeahirishwa.
Kwa Upande wa Simba waliotakiwa kucheza januari 3 na Mgambo JKT halafu januari 11 dhidi ya Mbeya City fc, mechi zao zimeahirishwa.
Timu zote nne zitamalizia mechi zao katikati ya wiki mara baada ya kombe la Mapinduzi kufikia tamati.
Comments
Post a Comment