DROO ya kombe la Mapinduzi 2015 imefanyika leo mjini Zanzibar na makundi yaliyopangwa kama ifuatavyo;
KUNDI A
Yanga SC, SC Villa, Polisi na Shaba ya Zanzibar
KUNDI B
Azam fc, KCC ya Uganda, KMKM na Mtende za Zanzibar
KUNDI C
Simba sc, Mtibwa Sugar ya Morogoro, JKU na Mafunzo za Zanzibar.
Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Januari Mosi mpaka 13 mwakani.
Siku ya ufunguzi, Wekundu wa Msimbazi wataanza kuoneshana kazi na Mtibwa Sugar saa 2:14 usiku.
Mechi hiyo itatanguliwa na mechi mbili za mapema baina ya JKU na Mafunzo na nyingine itawakutanisha Polisi dhidi ya Shaba.
Azam wataanza kampeni ya kusaka ubingwa januari 2 dhidi ya KCC na mechi hiyo itatanguliwa na mechi mbili baina ya KMKM na Mtende.
Yanga wao wataanza kurusha karata yao januari 3 mwaka huu kwa kuchuana na SC Villa majira ya saa 2:00 usiku.
Mechi hiyo itatanguliwa na mechi ya kundi C baina ya Mtibwa Sugar dhidi ya JKU.
Tutazidi kukupa ratiba zaidi ya michuano hiyo kupitia mtandao huu…
Comments
Post a Comment