SIMBA SC YAPATA PIGO ZENJ, MAGULI AUMIA



Na Bertha Lumala
Simba SC imepata pigo katika kambi yake Visiwani Zanzibra baada ya mshambuliaji wake hatari Elias Maguli kuumia.

Baada ya kuichapa Yanga SC mabao 2-0 katika mechi ya 'Mtani Jembe 2′ kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 13, kikosi cha wekundu hao wa Msimbazi klikwenda Zanzibar jana mchana kuiwekea kambi Timu ya Kagera Sugar FC kabala ya mechi yao inayofuata,
maguri
Simba SC itakuwa na kibarua kigumu mbele ya kikosi cha Mganda Jackson Mayanja cha Kagera Sugar FC watakapokutana katika mechi ya raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu huu itakayochezwa Uwanja wa Taifa Ijumaa.

Mratibu wa kambi ya Simba SC visiwani humo Abdul Mshangama amesema Maguli ameuamia kifundo cha mguu wakati wa mazoezi.

"Tunaendelea vizuri na mazoezi ingawa mshambuliaji wetu Maguli ameumia mguu. Wataalam wetu wa tiba wanamuangalia lakini taarifa za awali zinaonesha hatakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu," amesema.



Comments