SHINYANGA ‘DERBY’ YAMALIZIKA 3-3 KAMBARAGE


SHINYANGA 'DERBY' YAMALIZIKA 3-3 KAMBARAGE

a Bertha Lumala, Dar es Salaam
Timu za Stand United FC na Mwadui FC za Shinyanga zimetoka sare ya mabao 3-3 katika mechi maalum ya kirafiki kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani humo iliyoandaliwa kwa ajili ya kumaliza uhasama baina ya timu hizo.
11
Kumekuwa na uhasama mkubwa katika ya timu hizo baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuinyima kibabe Mwadui FC nafasi ya kupanda Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) licha ya kufuzu msimu uliopita wa Ligi Daraja la Kwanza (FDL) na kuipandisha kwa upendeleo Stand United FC.

Kutokana na uhasama huo, Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Muhibu Kanu amesema kuwa viongozi wa pande zote mbili walikutana na kuamua kuumaliza uhasama huo na timu zao zitachuana katika mechi hiyo ya kirafiki leo, ikiwa ni siku moja kabla ya Sikukuu ya Krismasi.

Stand United FC inayonolewa na Emmanuel Masawe iko nafasi ya 10 katika msimamo wa VPL ikwa na pointi tisa wakati Mwadui FC inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' inakamata nafasi ya kwanza katika msimamo wa Kundi B la FDL ikiwa na pointi 22 sawa na Toto Africans ya Mwanza.

Baada ya mechi hiyo, Kocha mkuu wa Mwadui FC amekimwagia sifa kikosi chake kwa kuishika timu hiyo ya Ligi Kuu na kuweka wazi kwamba Stand United FC kwa sasa imeimarika na anaamini itakuwa moto wa kuotea mbali VPL msimu huu.



Comments