Alan Irvine yuko kiti moto katika kazi yake West Brom
Tim Sherwood anapigiwa upatu zaidi wa kurithi mikoba ya Alan Irvine aliyetimuliwa kazi katika klabu ya West Bromwich Albion na uteuzi wake unaweza kutangazwa mwishoni mwa wiki hii.
Kocha huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur alibaki kidogo kupata kazi Hawthorns majira ya kiangazi mwaka jana, lakini mazungumzo yalivunjika kutokana na maslahi.
Sherwood anatamani kuwatumia wasaidizi wake Les Ferdinand na Chris Ramsey.
Kama atapata kazi hiyo, makocha wasaidizi wa timu hiyo Keith Downing na Rob Kelly watabaki kwenye sintofahamu.
Kocha wa zamani wa Tottenham Hotspur, Tim Sherwood anapewa nafasi kubwa ya kupata kazi West Brom
Comments
Post a Comment