Gareth Bale akiwa na makombe aliyoshinda tangu ajiunga na Real Madrid majira ya kiangazi mwaka 2013 ambayo ni (kutoka kushoto kwenda kulia) Kombe la klabu bingwa ya Dunia, Ligi ya mabingwa Ulaya, Kombe la Hispania na UEFA Super Cup.
MATUMAINI ya Manchester United kuinasa saini ya Gareth Bale yamegonga mwamba kufuatia Real Madrid kuda kamwe haitamuuza mshambuliaji huyo.
Louis van Gaal amekuwa akihusishwa na kufanya uhamisho mkubwa kwa Bale utakaogharimu paundi milioni 120 ambaye alisajiliwa majira ya kiangazi mwaka 2013 na miamba ya Hispania, Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya paundi milioni 86 akitokea Tottenham Hospurs.
Ripoti kutoka Hispania zinaeleza kuwa United walikuwa tayari kumsajili Bale, lakini Rais wa Real, Florentino Perez amedai nyota huyo mwenye miaka 25 hauzwi kwa bei yoyote ile.
Perez alisema: 'Sidhani kama Real Madrid itaenda bila Bale. Hatuwezi kusikiliza ofa yoyote bila kujali ni kiasi gani".
"Huyu ni mchezaji wa kipekee ambaye ametufaidisha mengi na ni muhimu sana kwa hatima ya baadaye ya klabu".
Comments
Post a Comment