Yohan Cabaye ameifungia Paris Saint-Germain (PSG) bao pekee dhidi ya Inter Milan na kumfanya Zlatan Ibrahimovic atoke kifua mbele kwa bosi wake wa zamani Roberto Mancini.
Ilikuwa ni mechi safi ya michuano ya kirafiki iliyopewa jina la Qatar Winter Tour, mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Le Grand Stade katika mji wa Marrakech nchini Morocco.
Kiungo huyo wa Kifaransa akafunga katika dakika ya 57 na kuipa PSG ushindi iliyoustahili.
Ibrahimovic na Mancini walikuwa na wasaa mzuri muda mfupi kabla ya mechi – vicheko na furaha pamoja na kushikana mikono – lakini mshambuliaji huyo wa Kiswidish, alionekana wazi kusaka ushindi kwa udi na uvumba dhidi ya kocha wake wa zamani.
Comments
Post a Comment