OKWI HATI HATI KUIVAA KAGERA SUGAR FC IJUMAA

okwi 2

Mshambuliaji anayetajwa kuwa 'mtukutu' wa Simba, Mganda Emanuel Okwi yuko hatarini kuikosa mechi yao inayofuata dhidi ya Kagera Sugar FC.

Simba SC iliyoweka kambi Visiwani Zanhzibar tangu jana mchana, itakuwa na kibarua kigumu mbele ya Kagera Sugar FC katika mechi ya raundi ya nane ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Ijumaa.Mratibu wa kambi ya Simba SC visiwani humo, Abdul Mshangama ameuambia mtandao huu kuwa Okwi anatarajiwa kujiunga na timu yao Alhamisi akitokea kwao Uganda alikoenda kwa ajili ya kufunga ndoa.

okwi 1
Okwi alifunga ndoa juzi na amekuwa na desturi ya kutorejea katika klabu anazosajiliwa wakati wa sherehe za Krismas ambayo ni siku yake ya kuzaliwa mwaka 1992.

"Okwi anatarajia kuja kuungana nasi Alhamisi," amesema Mshangama.
Kama Okwi atarejea nchini siku hiyo ya Sikukuu, nbi wazi kwamba hatakuwa na nafasi ya kukipiga katika kikosi cha kocha Mzambia Patrick Phiri cha Simba SC dhidi ya Kagera Sugar FC kwa sababu atakuwa na uchovu wa safari na atakuwa hajafanya mazoezi na timu.
Katika misingi ya weledi, mchezaji ambaye hajafanya mazoezi na timu, hastahili kupangwa katika mechi husika.
Katika hatua nyingine, Mshangama amesema wachezaji wengine wote wa Simba SC wakiwamo Waganda Simon Sserunkuma, Dan Sserunkuma, Joseph Owino na Juuko Murshid wameshawasili visiwani Zenj kujiandaa kwa mechi hiyo.
okwi
Kagera Suga FC inayonolewa na Mganda Jackson Mayanja, inakamata nafasi ya tano katika msimamo wa VPL ikiwa na pointi 11, mbili mbele ya Simba SC na itaingia kwenye Uwanja wa Taifa ikiwa na kumbukumbu ya kuifunga Yanga SC bao 1-0 katika mechi yao iliyopita


Comments