KOCHA mpya wa Simba sc, Mserbia Goran Kapunovic amewasili asubuhi ya leo majira ya saa 1:00 katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
Goran ametua kwa ndege ya Shirika la Qatar Airways na baada ya kuwasili amesema amekuja kufanya kazi na sivinginevyo.
Hata hivyo kocha huyo anayerithi mikoba ya Patrick Phiri amesema atazungumza mengi baada ya kumalizana na viongozi na kuanza kazi yake.
Goran anatarajia kuiongoza Simba kwa mara ya kwanza katika mechi za kombe la Mapinduzi linaloanza kutimua vumbi kesho januari mosi mwakani.
Comments
Post a Comment