Kocha wa Real Madrid mwitaliano Carlo Ancelotti amesema kitendo cha klabu yake kushinda taji la klabu bingwa dunia kimeifanya klabu hiyo kuumaliza vyema mwaka 2014 kwa kufanikiwa kushinda mataji manne ndani ya mwaka mmoja.
Mabingwa hao wa ulaya walifanikiwa kuwafunga mabingwa wa bara la Amerika Kusini San Lorenzo mabao 2-0 na kufanikiwa kutwaa taji hilo nchini Morocco,
Makombe mengine yalitwaliwa na Real mwaka huu ni Champions League, Copa del Rey na Uefa Super Cup.
"tumefanya vizuri sana mwaka huu,kamwe hautasahaulika,umoja wa timu hii ni kama familia ''.
Mwaka huu peke yake real Madrid imefanikiwa kufunga jumla ya mabao 178 kwenye mashindano yote na kuweka rekodi ya kufunga mabao mengi kwenye mwaka mmoja.
Comments
Post a Comment