Wapenzi wa burudani  ya                muziki wa kizazi kipya  watapata burudani ya fungua mwaka                kutoka kwa magwiji wa muziki wa kizazi kipya ambao                wanatamba nchini katika tamasha la  wazi la maisha murua                na Vodacom katika ufukwe wa Coco beach jijini Dar es                Salaam.Baadhi ya magwiji hao ni Profesa J,Temba,Chege,Roma                Mkatoliki na wengineo wengi.
        Tamasha hili                 litakalokutanisha magwiji wa bongo fleva ambalo limeanza                kuwa gumzo la  jiji kutokana na kuwa na burudani za aina                mbalimbali kwa ajili ya kukonga nyoyo za wapenzi wa                burudani  limeandaliwa na Vodacom Tanzania.
        Meneja Uhusiano wa Umma                wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amesema kuwa Vodacom                imeamua kuandaa tamasha hili la"Vodacom Maisha ni Murua"                kwa ajili ya kuwapatia furaha na burudani wateja wake na                 wananchi kwa ujumla katika sikukuu ya  mwaka mpya                vilevile wananchi watapata fursa ya kujinunulia bidhaa                mbalimbali za huduma za Mawasiliano kwa gharama nafuu.
        "Kama ilivyo kauli mbiu                yetu kuwa "Ukiwa na Vodacom maisha ni murua"tunahakikisha                mbali na kutoa huduma bora kwa wateja wetu pia tunajua                kuwa kuna muda wanahitaji kufurahi kwa burudani  hivyo                ndio maana tunaandaa na kudhamini matamasha ya  aina hii                na tutaendelea kufanya hivyo siku zote ikiwa ni moja ya                njia ya kusema ahsante kwa wateja wetu kwa kutuunga                mkono"Alisema.
        Alisema mwaka huu                burudani kupitia matamasha haya imekuwa jijini Dar es                salaam  wakati mikakati inafanyika kuhakikisha burudani                hii inasambazwa kwa wateja wote nchi nzima "Tunawajali na                kuwasikiliza wateja wetu ambao kwetu ni wafalme hivyo                tutahakikisha huduma bora na burudani katika kipindi                maalum kama hiki inawafikia katika siku za usoni".Alisema                Nkurlu.
        
Comments
Post a Comment