MNENGUAJI ALLIYAH WA FM ACADEMIA ANAPOKUNG’UTA BASS GITAA


MNENGUAJI ALLIYAH WA FM ACADEMIA ANAPOKUNG'UTA BASS GITAA
MNENGUAJI ALLIYAH WA FM ACADEMIA ANAPOKUNG'UTA BASS            GITAA

Moja ya mambo ya kuvutia kwenye onyesho la Mapacha Watatu na FM Academia Ijumaa iliyopita pale Mzalendo Pub, ni dansa wa kike Alliyah wa FM Academia kukung'uta gitaa la bass.

Mwanadada huyo katika moja ya nyimbo za bendi yake, akashika mpini wa bass gitaa na kulicharaza katika hali ambayo ilifurahisha mashabiki wengi.

Kuna uhaba mkubwa wa wapiga ala wa kike na hivyo ujio wa Alliyah na bass gitaa, ni jambo kutia moyo.

Katika kuonyesha kuwa dansa huyo amedhamiria kufanya mengi, akashiriki pia kuimba wimbo Dunia Kigeugeu na kuimba kipande kilichorekodiwa na Miraeza.



Comments