Serikali ya Guinea ya Ikweta, wenyeji wa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2015 imefikia hatua nzuri kuhakikisha hakutokei maambukizo zaidi ya virusi vya Ebola, kwa kutangaza hatua zinazochukuliwa ili michuano hiyo isikumbwe na mlipuko wa ugonjwa huo.
Baadhi ya wachezaji wa Kiafrika na timu zao za nje zimeonesha hofu kwamba huenda michuano hiyo ikasababisha kulipuka zaidi kwa maambukizi mapya, sababu kubwa ikitajwa kuwa idadi kubwa ya mashabiki watakaokwenda kushuhudia mechi hizo.
Hata hivyo, Guinea ya Ikweta imesema mikakati imefanywa na inazidi kufanywa kuzuia maambukizi ya Ebola yanayotishia uhai wa fainali hizo zitakazofanyika kuanzia Januari 17 hadi February 8. Mikakati hiyo mni pamoja na;
"Wasafiri wote wanaowasili Uwanja wa Kimataifa wa Malabo kutoka nje watapimwa afya, hasa joto.
"Wasafiri wanapigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole, hivyo ni rahisi kuwatambua pindi kukitokea tatizo lolote.
"Watu wote wanaosafiri na kuingia nchini humo wanaandikishwa na taarifa zao zao za afya kuingizwa kwenye fomu maalum na kupatiwa vyeti vya utimamu wa afya zao.
"Na mashabiki wote kwenye viwanja watakuwa wanavaa vifaa maalum mikononi kuzuia uwezekano wa kuambukizwa Ebola kupitia kushika milango na vifaa vya utambuzi wa tiketi vilivyopo uwanjani.
Mwisho, madaktari 30 kutoka Cuba, ambao wanatoka kitengo maalum cha magonjwa ya milipuko 'specialists in epidemiology', tayari wameshaingia Guinea, na watakuwapo hadi mwisho wa michuano hiyo.
Comments
Post a Comment