Kushoto ni mwimbaji tegemeo wa Twanga Pepeta Dogo Rama na kulia ni mwimbaji na rapa wa bendi hiyo, Msafiri Diouf wakionyesha kuwa ushirikiano wao sio jukwaani tu bali hata nje ya jukwaa.
Pichani kama walivyokutwa na kamera ya Saluti5 hivi karibuni kwenye viwanja vya Leaders, wasanii hao wanapata nyama choma juu kwa juu wakiwa hawana hata muda wa kukaa vitini pengine kutokana na namna kazi zilivyowabana.
Picha hii ilipigwa Jumapili, siku ambazo Twanga Pepeta hutumbuiza Leaders Club.
Comments
Post a Comment